Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mtoto wa wiki moja aokotwa vichakani

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki moja hadi wiki Mbili amekutwa ametelekezwa vichakani katika kitongoji cha nyambogo kijiji cha nyakafuru wilayani Mbogwe mkoani Geita hali ambayo imezua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

Akisimulia tukio hilo Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Marry Lumambo mkazi wa kijiji hicho amesema alikuwa ameenda kujisaidia kichakani lakini ghafla akasikia sauti ya mtoto mchanga akilia ndipo akawaita majirani wakaanza kumtafuta na kumkuta mtoto huyo ndipo wakamchukua na kumpeleka polisi na kuambiwa amlee.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa ustawi wa jamii halimashauri ya wilaya ya Mbogwe Diana Mwinuka amekiri kupokea taarifa za tukio hilo huku akisema wamefanya jitihada za mapema za kupata maziwa ya mtoto huyo ili kuokoa maisha ya kichanga hicho.

Nao baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamelaani tukio hilo huku wakiiomba serikali kuchukua hatua kali pindi atakapo bainika mtu aliyemtupa mtoto huyo ili iwe fundisho kwa wananchi wengine kwani kufanya hivyo ni ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *