Mtoto wa Rais Joe Biden ashitakiwa

Mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden , Hunter Biden jana Alhamisi amefunguliwa mashitaka na viongozi wa mashitaka, akituhumiwa kununua bunduki katika muda aliokiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine, wakati akidanganya kuwa hakuwa akitumia, ili aweze kuuziwa.

Mashitaka hayo dhidi ya Hunter mwenye umri wa miaka 53 mara moja yamezua mjadala mpya kwenye kampeni za rais wa Marekani mwaka ujao. Baba yake Joe Biden anapanga kuwania tena urais wakati mpinzani wake mkuu wa Repablikan, Donald Trump akikabiliwa na mashitaka manne ya jinai, yenye jumla ya kesi 91 za kusikilizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *