Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi ya Uganda (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo, mwaka 2031.
Jenerali Muhoozi ambaye amezoeleka kwa kuchqpisha maandiko yenye utata, amesema ana imani thabiti ya kuibuka na ushindi wa kishindo kwa zaidi ya asilimia 90 kupitia uungwaji mkono na ushawishi wa baba yake.

Amekuwa akitajwa mara kadhaa kama mtu anayeandaliwa kuchukua mikoba ya utawala kutoka kwa baba yake, ambapo katika uchaguzi wa Januari 2026 alitangaza kugombea kabla ya kubadili uamuzi huo.


