MTOTO WA MUSEVENI AZUA UTATA MAPIGANO DRC

Mkuu wa jeshi nchini Uganda, ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba ameibua mjadala tata kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kudai Jeshi la nchi hiyo au waasi wa M23 wataingia katika mji wa Kisangani nchini DRC wiki ijayo.

Kupitia chapisho lake la kwenye ukurasa wake wa X, Kainerugaba amesema jeshi lake au waasi wa M23 wataingai katika mji huo kwa agizo la Rais Yoweri Museveni, ili kuwaokoa wakaazi wa mji huo.

Wanajeshi wa Uganda wamekuwa nchini DRC, wakishirikiana na jeshi la FARDC, kupambana na makundi yenye silaha wakiwemo waasi wa CODECO na ADF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *