Mtoto wa Mr. Ibu atuhumiwa kufanya wizi

Mtoto wa kike wa kuasili wa msanii wa Mr. Ibu aitwaye Jasmine Okekeagwu, ametuhumiwa kufanya wizi wa akaunti ya mtandao wa kijamii wa TikTok ya Mr Ibu ambaye amafariki na kuandika jina lake.

Akaunti ya Mr. Ibu ambayo ina wafuasi milioni 1.3, sasa ameweka jina lake Lady Jasminec., kitu ambacho kimeibua hisia kali za watu mitandaoni kutokana na kitendo hicho kilichofanywa.

Mwezi Januari mwaka huu, Onyeabuchi Okafor ambaye ni mtoto wa kiume wa Mr Ibu na Jasmine mtoto wa kuasili, walikamatwa na polisi nchini humo kwa madai ya kuiba fedha zilizokuwa zikichangishwa kwa ajili ya matibabu ya muigizaji huyo ambaye amefariki jana Machi 2, 2024.
Watoto hao walidaiwa kuingia kwenye mifumo ya benki kwa kutumia simu ya muigizaji huyo waliyokuwa wakiimiliki na kuiba Naira 55 milioni ambazo ni zaidi ya TSh/=88.3 milioni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *