Mtoto mwingine ametolewa Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera na kwenda kuinasa na kisha kuitoa ambayo alikuwa akiichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni siku nne zilizopita na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka.
Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima amesema mtoto huyo alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa sana na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.