Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia kijana aitwaye Humphrey Francis Kihali [25] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi aitwaye Francis John Kihali [50] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Septemba 10, 2023 majira ya saa 10:45 jioni eneo la Ilemi mtuhumiwa huyo alimvizia baba yake mzazi Francis John Kihali akiwa chumbani kwake na kisha kumpiga kwa kutumia ubao na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na kufariki dunia Septemba 11, 2023 majira ya saa 1:30 asubuhi.
Pamoja na uchunguzi wa awali kubainisha kuwa mtuhumiwa huyo ana tatizo la akili, jeshi la polisi mkoani Mbeya limesema uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.