Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamezindua jezi mpya zitakazotumika kwa ajili ya timu zote za taifa.
TFF wamezindua jezi hizo zitakazotumika katika Mashindano ya AFCON 2024 nchini Ivory Coast pamoja na mashindano mengine ambayo timu hizo za taifa zitashiriki.