Mtibwa wamtimua Kondo

Klabu ya Mtibwa Sugar imemfuta kazi kocha Habib Kondo kama kocha mkuu klabuni hapo kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo ambayo mpaka sasa haijashinda mechi yoyote kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.

Wakata Mtibwa wamepoteza mechi 3 na sare mbili katika michezo mitano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara mpaka sasa msimu huu 2023/24. Zipo tetesi kwamba aliyekuwa kocha wa Ihefu FC, Zuber Katwila maarufu kama ‘Mbaya wa Yanga’ anatarajiwa kuchukua mikoba ya Kondo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *