Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeusogeza mbele mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga SC na Simba SC ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 15, 2025 kuanzia saa 11:00 jioni.
Mchezo huo sasa utafanyika Juni 25, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni, ambapo Bodi imezitakia maandalizi mema klabu hizo.

