Mtafutaji Asiyechoka Aliyebeba Kombe akiwa na Mika 66,Siku 117

Na Ibrahim Rojala

Usiku wa Mei 23,2024 ulipambwa na historia tamu na chungu kwa timu mbili zilizokutana katika fainali ya Kombe la Europa ambayo iyakutanisha Mataifa mawili ambayo ni Ujerumani na Italia kupitia timu za Bayer Leverkusen na Atlanta ambapo karata za wapenda soka wengi zilitupwa kwa Leverkusen ambayo hadi inaingia katika mchezo huo ilikuwa imecheza michezo 51 bila kufungwa msimu huu,baba wa umri wa miaka 66 alikuwa akiwaongoza vijana wake kupambana na vijana wa kijana wa miaka 42 katika dimba la Dublin huko Jamhuri ya Ireland.

Kuna wanaume watatu ambao mchezo huo hautofutika kirahisi vichwani mwao,wa kwanza ni Raia wa Nigeria na Mshambuliaji wa Klabu ya Atlanta Ademola Lookman ayefunga hat-trick wakati Atlanta ikiichapa Bayer Leverkusen 3-0 na kushinda taji la Ligi ya Europa.

Wapili ni kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ambaye historia yake nzuri ya kuiongoza timu hiyo katika michezo 51 bila kufungwa iliishia hapo kwa kuambulia kichapo,kupoteza kombe na matumaini ya kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja.

Aliyebeba kumbukumbu muhimu zaidi kwake binafsi na yenye funzo kwa vijana tunaoshindwa kugangamala ni kocha wa Atlanta, mzee ambaye akiwa na umri wa miaka 66 na siku 117, Gian Piero Gasperini hatimaye ameshinda kombe la kwanza la kazi yake ya usimamizi.

Safari ya kuelekea mafanikio kwa mzee huyu aliyeanzia kazi yake ya ukocha katika timu ya vijana ya Juventus mnamo mwaka 1994 imebeba mafunzo mengi kwa wale tulio na tabia ya kukata tamaa.

Babu Gasperin baada ya kukaa kwa muda mrefu na vijana wa Juventus mwaka 2003 aliamua kuondoka ndani ya miamba hiyo na kujiunga na timu ya Crotone iliyokuwa ikishiriki Ligi ya Serie C1na kuipandisha hadi Serie B kabla ya kutimuliwa.

Mtafutaji hachoki, Kuanzia 2006 akawa kocha mkuu wa klabu ya Genoa, na alikiongoza kikosi chake kupandishwa daraja hadi Ligi kuu ya Italia (Serie A) katika msimu wake wa kwanza.

Basi Bwana safari yake ya ukocha mwaka 2011 ilihamia katika kikosi cha Inter Milan ambayo alijiunga nayo mwezi Juni lakini hata hivyo alitimuliwa kazi Septemba 21ya mwaka huo huo baada yakuwa na mfululizo wa matokeo mabaya baada ya katika mechi tano kupigwa katika mechi nne na kutoa sare moja.

Mnamo Septemba 16, 2012, Gasperini alitangazwa kama meneja mpya wa Palermo, timu yake ya zamani aliyowahi kuitumikia kama mchezaji, akichukua nafasi ya Giuseppe Sannino,akafukuzwa mnamo Februari 4,2013 baada ya kupigwa 2-1 na Atlanta ambayo ndiyo aliyoweka nayo historia ya kubeba nayo kombe lake la kwanza katika maisha yake ya ukocha.

 Februari 24, 2013 Gasperini aliajiriwa tena kama meneja wa Palermo, akichukua nafasi ya Alberto Malesani baada ya kuisimamia michezo mitatu,tarehe 11 Machi 2013, Gasperini aliondolewa tena kutoka wadhifa huo hakukata tamaa kwani alirudi tena Genoa

Mnamo tarehe 29 Septemba 2013, Genoa ilitangaza kumuajiri tena Gasperini baada ya kupita miaka mitatu tangu walipomuajiri na kumfukuza kwa mara ya kwanza na yupo ndani ya klabu ya Atlanta tangu 2016 kabla ya usiku wa Mei 22,2024 kulipa hisani ya uvumilivu na kugangamala kwa wamiliki wa timu hiyo kwake kwa kutwaa taji lake la kwanza ambalo ni Uefa Uropa Champions League.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *