MTAALA MAALUM WA ALPHA KUSAIDIA KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI KAHAMA

Na William Bundala, Kahama – Shinyanga.

Huduma ya maendeleo ya ukuaji wa mtoto na kijana ya Compassion Cluster Kahama imeanzisha mtaala maalumu wa Alpha unaolenga kuwasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuwaongoza kumjua Yesu, hatua inayotajwa kusaidia kupunguza tatizo la watoto wa mitaani katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtaala huo uliofanyika katika Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Kahama Mjini, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto wa mitaani katika manispaa hiyo.

Nkinda amesema ili kutokomeza tatizo hilo, wazazi na walezi wanapaswa kusimamia wajibu wao wa malezi na kuhakikisha watoto wanapata uangalizi unaostahili tangu wakiwa wadogo.

“Suala la watoto wanaoishi katika mazingira magumu lipo kwa kiwango kikubwa katika wilaya yetu,sasa ni jukumu la wazazi na walezi kusimamia kwa ukaribu malezi ya watoto tangu wakiwa wadogo,hii itasaidia mtoto kukua katika maisha mazuri ya kiroho na kimwili.” Amesema Nkinda.

Kwa upande wa Compassion, mmoja wa maofisa wa shirika hilo amesema zaidi ya vijana laki moja wanahudumiwa na taasisi hiyo nchini Tanzania, huku takribani vijana 3,500 wakihudumiwa katika Mkoa wa Shinyanga ambapo vijana hao hupatiwa huduma mbalimbali za msingi zikiwemo elimu, malazi, mavazi pamoja na malezi yanayowajengea maisha bora ya baadaye.

“Compassion yetu inahudumia zaidi ya vijana laki moja nchini Tanzania,na kwa upande wa mkoa wa Shiyanga inahudumia takribani vijana elfu tatu mia tano ambao tunawapatia elimu, malazi, mavazi pamoja na malezi yanayowajengea maisha bora.” Amesema afisa huyo.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, mmoja wa vijana wa huduma hiyo, Happyness Daniel, amesema lengo la mtaala wa Alpha ni kuwakutanisha vijana na kuwasaidia wale wanaovutwa na mambo ya dunia kurejea katika misingi ya maadili mema.

“Mh mgeni rasmi lengo kubwa la mtaala huu wa alfa ni kuwakutanisha vijana na kuwasaidia wale wanaovutwa na mambo ya dunia kurejea katika misingi ya maadili mem ana hii inatusaidia kwa kiasi kikubwa vijaa kubadilika na kujikuta tupo katika misingi imara ya kiriho na kimwil,i” amesema Happyness.

Kwa upande wao, Stephania Gabriel na Lucy Macheyeke wamesema malezi ya mtoto huanza tangu hatua za awali kabisa na yanahitaji ushirikiano wa wazazi wote wawili, baba na mama.

“Ni ukweli usiopingika kuwa malezi ya mtoto huanza tangu hatua za awali za makuzi ambapo baba na mama wanahitaji ushirikiano wa Pamoja katika kusaidia malezi kwa watoto a hii itasaidia watoto kukuwa wakiwa na malezi bora kila wakati,” smesema Bwana Gabriel na Bi Macheyeke.

Wamesisitiza kuwa msingi wa maadili ya mtoto hutegemea namna wazazi walivyolelewa na jinsi wanavyoishi, hivyo jamii inapaswa kuwekeza zaidi katika malezi bora ya watoto ili kujenga kizazi chenye maadili na uwajibikaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *