MSISITIZO: ACT – WAZALENDO HAINA MGOMBEA WA URAIS UCHAGUZI WA 2025 – INEC

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imeuarifu umma kuwa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT –
Wazalendo) hakina wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Taarifa iliyotilewa na INEC hii leo Septemba 22, 2025 imeeleza kuwa ACT – WAZALENDO haina wagombea hao kwa kuzingatia uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wa
Septemba 15, 2025 uliotengua uteuzi wa Luhaga Mpina aliyependekezwa na Chama hicho kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *