MSIPUUZE ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA – SHEIKH NASSOR

Na Saulo Stephen – Singida.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassor amewataka waumini wa dini ya Kiislamu mkoani humo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftari la mpiga kura awamu ya pili na kuacha kupuuza juu ya zoezi hilo lililoanza Mei 16-22,2025.

Shekh Issa ametoa rai hiyo wakati akiongea na waumini wa dini hiyo kwenye swala ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti uliopo mji wa mdogo wa Ilongero wilaya ya singida vijijini ambapo amesema ni muhimu kujiandikisha katika daftari hilo ili kuweza kushiriki katika Uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais.

Amewasihi wazazi na walezi wa Kiislamu mkoani Singida wenye watoto ambao wamefikisha umri wa miaka 18 wawahimize na kuwasimamia ili kuhakikisha wanajiandikisha katika daftatari hilo ili kuwa na sima za kuweza kupiga kura kwani nafasi hiyo ni ya muhimu kwao hivyo wanapaswa kuichangamkia kwa kuhakikisha wanajiandikisha sanjari na kuboresha taarifa zao.

Aidha katika hatua nyingine shekh Issa amewataka waumini wa Kiislamu mkoani Singida kuhitaji kuhubiri na kuilinda amani ya mkoa huo kwa kutojihusidha na vitendo vinanvyoashiria uvunjifu wa amani na badala yake kuwa mabalozi wazuri wakusaidiana na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo jeshi la Polisi mkoani humo kwa kukomesha na kutokomeza vitendo visivyofaa mkoani Singida.

Amesisitiza kuwa uwepo wa amani uliopo katika mkoa wa Singida ndio chanzo cha waumini hao kupata nafasi ya kufanya ibada pasipo bugudha yoyote pamoja na kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo yao hivyo wana kila sababu ya kuilinda amani hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *