MSILETE MCHEZO NA AMANI YA NCHI – MAYALA

Na Saada Almasi, Bariadi  – Simiyu.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya udiwani Kata ya Kasoli, Mayala Lucas amewataka Wananchinwa kijiji cha Mwamlapa kilichopo Wilayani humo, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani madhara yake ni makubwa.

Ameyasema hayo akiwa kijijini hapo katika muendelezo wa ziara zake ya kijiji kwa kijiji kuomba kura na ridhaa kwa wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Oktoba 29 mwaka huu na kuwasisitiza kuwa madharq ya machafuko huwakumba zaidi wanawake kuliko wanaume.

“Amani tuliyonayo ilipiganiwa na Mwalimu Nyerere na hadi leo hatujawahi kuingia katika machafuko lakini ajabu watu wanaopinga serikali wanahamasisha kuacha kupiga kura mkaandamane niwaambie madhara tutakayoyapata muhanga mkubwa ni mama kwani yeye ndiye mtu pekee hawezi kukimbia bila kubeba watoto wake,bab atakimbia ataacha kila aokoe uhai wake,” amesema Mayala.

Ameongeza kuwa, endapo yakitokea machafuko jeshi ndilo litachukua utawala wa nchi hali ambayo itakuwa mbaya zaidi kwani hatutokuwa na maamuzi.

Sambamba na hilo, Mayala amewahakikishia wananchi hao kuwa miaka mitano ambayo alipewa ridhaa ya kuongoza kata hiyo imefanya mengi na bado Serikali inaendelea kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na kodi yake

“Kulikuwa na ukosefu wa maabara kwa wananfunzi wa sekondari katika kipindi cha uongozi wangu tumejenga na inatumika,badhi ya maeneo hayakuwa yameunganishwa na barabara lakini sasa yameunganishwa hiyo ni hatua kubwa japokuwa hatujaishia hapo lengo ni kusogeza huduma zaidi ili kila mwananchi aione kodi yake,” ameongeza Mayala.

Kufuatia suala la upungufu wa maji katika kijiji cha Busese Mayala amewaahidi wananchi hao kutoa ushirikiano wa dhati na kuongeza pampu za maji huku akimtaka mwenyekiti wa kijiji hicho kutoa ushirikiano na wanakijiji hao ili kutambua vyanzo vya maji.

“Eneo la kijiji hiki ni kubwa watu ni wengi ili tujue kuwa mahali gani kuna maji niombe ushirikiano zaidi kumpatia mwenyekiti mtambue vyanzo vya maji ili tuwasogezee pampu,” amesema Mayala.

Akihitimisha ziara yake katika kijiji hicho amemuombea kura mgombea nafasi ya Ubunge Masanja Kadogosa amewaambia wana Kasoli kuwa kati watu wenye mapenzi mema na kata hiyo ni pamoja na Kadogosa ambaye amedhamiria kuunganisha maeneo yote kwa barabara ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia maendeoleo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *