Mshukiwa wa mauaji ya Watoto wanne huko Ggaba nchini Uganda, Christopher Okello Onyum (39), ambaye alifanya mauaji hayo katika Kituo cha Mpango wa Maendeleo ya Watoto jijini Kampala, amefikishwa Mahakamani.
Amefikisha Mahakamani hapo hii leo Aprili 7, 2026 kwa mashtaka ya mauaji baada ya kukamatwa kwake Aprili 2, 2026 kufuatia kujitambulosha kama mzazi anayetaka kuandikisha watoto na baada ya kulipa ada alijifungia darasani na kuwakata mapanga watoto wanne.

Onyum, aliwasili Mahakamani chini ya ulinzi mkali wa maafisa usalama wenye silaha, huku watu wakifurika kushuhudia mtuhumiwa huyo aliyefanya tukio la kushtua wengi.
Aliwasilishwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Aidah Nanjala kisha kusomewa mashtaka yanayomkabili.
