Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ghana, Black Stars, Raphael Dwamena (28) amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani leo wakati wa mechi kati ya timu yake ya Egnatia Rrogozhine ya nchini Albania dhidi ya Partizani.
Mtandao wa soka wa Citi Sport umeripoti kuwa kifo chake kimetokea baada ya mchezaji huyo kupata mshtuko wa moyo dakika ya 23 ya mchezo na kusababisha kusimamishwa kwa mchezo huo.