
Msanii kutoka kundi la Wasafi D VOICE amelalamika kuhusu fitna za muziki anazofanyiwa na watu ambao hawafahamu kwa kushusha kazi zake za Muziki kwenye mitandao yake ya Kijamii na Zaidi Youtube.

D Voice kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ujumbe huu ‘’Nilitamani Watu Wajue Mziki Nikazi Yangu Mbayo Mimi Binafsi Na Iheshimu Kwa Sababu Imeshikilia Nafasi Kubwa Ya maisha Yangu Kinapotekea Kikundi Cha Wapuuzi Wachache Wakashikana Masikio Nakuanzaa Kushusha Nyimbo Zangu Bila Kigezo Maalumu Wala Sababu Ya Msingii Hii Inakuwa Hai Sound Good Hii Ni Mara Ya Pili Kwenye Album Yangu Mlishusha Nyimbo Zanju Mbili Nikapambana Zikarudi Hii Wa sasabivi Nikikugundua Utalipa Gharama Ambazo Haujawahi Kulipishwa Kwenye Haya Maisha Yako’’ – D Voice.

D Voice kwa sasa ndiye msanii wa mwisho aliyetambulishwa na lebo ya Wasafi Zaidi ya miezi 11 iliyopita.


