MSALALA DC YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA WATUMISHI

Na William Bundala, Msalala – Kahama.

Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imeendesha zoezi la upimaji  wa hali ya lishe, msukumo wa damu pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu kwa watumishi wa makao makuu kwa kwa lengo la kulinda afya za wafanyakazi ili kuongeza ufanisi mahali pa kazi.

Akizungunguza wakati zoezi hilo, Mwamini Mziray ambaye ni afisa lishe wa Wilaya ya Msalala amesisitiza juu ya ulaji wa mlo kamili wa chakula kwa kuzingatia makundi yote sita ya chakula,na kufuata mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi.

“Zingatieni ulaji wa mlo kamili wa chakula kwa kuzingatia makundi yote ya chakula,na muepuke ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi,sukari na msipende kula vyakula vyenye chumvi nyingi na zingatieni kufanya mazoezi mara kwa mara,” amesema Mziray.

Sambamba na hayo Bi,Mziray amewataka watumishi kuepuka matuminzi ya pombe, sigara na tumbaku Pamoja na kuepuka msongo wa Mawazo na kupima afya mara kwa mara.

“Ni muhimu kupima afya mara kwa mara hii itasaidia ugonjwa kugundulika mapema hivyo kuweza kutibika, pia kugundua Kama uko katika Hatari ya kupata au unaviashiria hatarishi vya magonjwa sugu,lakini zaidi epukeni matumizi ya Pombe,sigara na tumbaku pia msiruhusu msongo wa Mawazo,” ameongezea Bi. Mziray.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi wa wameupongezi uongozi wa halmashari ya Msalala kwa uamuzi wa kupima afya za watumishi na kwamba watazingatia mambo yote muhimu ikiwemo unywaji wa pombe na kuzingatia mazoezi.

“Tunashukuru uongozi kwa maamuzi ya kutupima afya,hii imetusaidia kujua hali zeu za kiafya na kujua mambo gani ya kuzingatia,Tutazingatia yote tulioshauriwa ikiwemo unywaji wa pombe na kuzingatia mazoezi,” Wamesema baadhi ya watumishi.

Zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza limefanyika leo Oktoba 22, 2025 katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na linatarajiwa kua endelevu ili watumishi wote waweze kufikiwa na huduma hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *