Msaada wa Dawa na vifaa tiba vyafika Hanang

Awamu ya kwanza ya ugawaji wa vifaa tiba na dawa vilivyotolewa na Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Hanang imewasili katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini).

Meneja wa Kanda ya MSD Kilimanjaro Rehema Shelukindo ameeleza kuwa, vifaa hivyo ni pamoja na maji tiba (drips), dawa za kutibu magonjwa ambukizi na mengineyo (antibiotics), dawa za maumivu na mashuka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa MSD itaendelea kupeleka bidhaa za afya katika eneo hilo kadri itajavyoelekezwa na Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *