MRISHO GAMBO AMJIBU MAKONDA, MADAI YA KUTOHUDHURIA VIKAO…..

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amejibu hoja ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ya kudai haudhurii vikao, mbunge huyo amesema suala hilo linahitaji elimu kwa sababu yeye ni mbunge na ana vikao vya Bunge.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gambo amesema ‘ Ile ziara haikua ya mkuu wa mkoa, ule mkutano haukua wa Mkuu wa Mkoa, ilikua ziara ya Waziri wa Ujenzi na mimi nilimuuliza Waziri wa Ujenzi, niletegemea yeye ndiye atoe majibu ya hoja nilizojenga,nikaona Makonda ametoa majibu ambayo kimsingi hayakuhusiana na hoja nilizojenga, ni lazima afahamu mimi sio mfanyakazi wa serikali, Mimi sio mtumishi wa serikali ,Nina utaratibu wa kufanya kazi kulingana na katiba mimi ni mwakilishi wa wananchi, Mimi ni mbunge wa Bunge la Tanzania’ – Gambo.

‘Nina vikao vya kisheria navyotakiwa kuhudhuria ikiwemo vikao vya Bunge pamoja na kamati zake, sidhani kwa nafasi yake kama ni sehemu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ – Gambo

Jumatatu ya Jana, Januari 6, 2025 wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyekuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa- Sambasha- Tumbolo ya kilomita 18 kwa thamani ya Sh23 bilioni, Makonda alidai Gambo haudhurii vikao.

Makonda alisema hayo, baada ya Gambo kuelezea changamoto za barabara za Mkoa wa Arusha, akimuomba Waziri Ulega ampatie majibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *