MRADI WA LISHE BORA WAZINUFAISHA SHULE TATU ZA SEKONDARI SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Katika kuboresha hali ya lishe na upatikanaji wa Chakula cha uhakika kwa Wanafunzi pindi wawapo shuleni, Shule tatu za Sekondari Mumbii, Mughamo na Itaja za Wilaya ya Singida Vijijini, zimenufaika na mradi wa lishe Bora kupitia ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Action Against Hunger.

Akizungumza wakati alipotembelea shule hizo kujionea miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe amelishukuru Shirika hilo la Action Against Hunger kwa kutekeleza miradi hiyo katika shule hizo za Sekondari, ambapo kwasasa zimekuwa zikilima bustani za mbogamboga kupitia mfumo wa mwagiliaji na hivyo kuwa na uhakika wa mboga kwa ajili ya chakula pindi wawapo shuleni.

Aidha DC Gondwe ameshukuru mchango wa shirika hilo, kwa kujitoa na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanapata lishe bora wakiwa shuleni, ili kuwaimarisha kiakili na kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo yao huku akiwasisitizia viongozi na wananchi wa kata hizo, kuendelea kuhamasika na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni.

Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa wilaya ya Singida ameongoza na Katibu Tawala wa Wilaya, Naima Chondo na mwakilishi wa shirika la Action Against Hunger – USA, Hillary Makundi vilevile wataalamu kutoka katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *