Mr. Ibu atazikwa Juni 28, mwaka huu

Shughuli za mazishi za nguli wa filamu kutoka Nigeria, John Okafor, maarufu kama Mr. Ibu zinatarajiwa kufanyika Juni 28 ya mwaka huu.


Taarifa hiyo imetolewa na kaka yake Sunday Okafor ambaye amesema shughuli za kuaga mwili wa msanii huyo zitaanza Juni 25 hadi siku ya mazishi Juni 28, kabla ya mazishi yake kufanyika nyumbani kwake katika mji aliozaliwa wa Amuri, magharibi katika jimbo la Enugu.

Akielezea kuchelewa kuzikwa kwa mwigizaji huyo, Sunday Okafor alibainisha kuwa mwigizaji huyo mashuhuri atapewa sherehe yake ya mwisho kishujaa, inayolingana na hadhi yake hivyo basi kucheleweshwa kwa mazishi.

Mr.Ibu alifariki Machi 2,2024 akiwa na umri wa miaka 62 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Evercare na aliwahi kutamba katika filamu mbalimbali kama vila Aki na Ukwa, Chop Money na The Collaborator.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *