Mwigizaji maarufu kutoka Nigeria, John Okafor, maarufu kama Mr Ibu, amelazwa hospitalini hivi karibuni na anaomba msaada wa kifedha kutoka kwa Wanigeria ili kulipia bili zake za matibabu.
Katika video aliyoweka Instagram msanii huyo ameeleza kuwa kuwa yuko katika hatari ya kukatwa mguu ikiwa hawezi kupokea matibabu yanayofaa kwa haraka.