Mr Eazi kumshitaka producer wake

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Mr Eazi, ametishia kumshitaka mtayarisaji wa muziki kwa kushindwa kufuata mkataba wao.

Kwa mujibu wa Mr Eazi anasema kuwa, alimlipa mtayarishaji huyo ambaye jina lake halikutajwa kiasi cha $5,000 sawa na Tsh/=12,490,000.19 kutengeneza wimbo ambao alitarajia uwepo kwenye albamu yake ya, ‘The Evil Genius’, iliyotoka hivi karibuni lakini hakuwahi kumtumia wimbo huo.

Eazi amesema hatajali kutumia $100,000 sawa na Tsh/=249,800,003.87 kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtayarishaji huyo na atafanya hivyo siku ambayo “atakuwa na kuchoka.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *