MPINA APENDEKEZWA NA ACT WAZALENDO KUWANIA URAIS BARA

Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT – Wazalendo imewapendekeza Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina kuwania kugombea urais kwa upande wa Tanzania Bara.

Aidha kwa upande wa Zanzibar, ACT kimempendekeza mwanachama pekee aliyechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Othman Masoud Othman.

ACT kimeeleza kuwa, kimefikia hatua hiyo baada ya kimepokea na kuridhia hatua ya kiongozi wake, Dorothy Semu kujitoa kugombea urais wa Tanzania.

Semu aliieleza Halmashauri Kuu kuwa amechukua hatua hiyo katika kutekeleza wajibu wake wa kiuongozi, ili kukiwezesha chama kuiondosha CCM madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *