Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameielekeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha mpango wa Taifa wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) unasainiwa ndani ya wiki hii na wiki ijayo unaenda katika mikoa na Halmashauri zote nchini kwaajili ya utelezaji.

Mpanju ametoa maelekezo hayo leo Disemba 14,2023 Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa Kitaifa wa Wadau wa mpango wa sekta zote ambapo kiliambatana na uzinduzi wa Mwongozo Jumuishi wa Taifa wa Utekelezaji wa Mpango huo siku ya kwanza.
Sambamba na hilo Mpanju amesema kuwa kupitia Wizara hiyo Serikali imetoa rai kwa watekelezaji wa mpango huo kuhakikisha wanasimamia vyema mipango yote waliojiwekea inatekelezeka kikamilifu. Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya mtoto kutoka wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema kuwa lengo kuu la kuandaa mpango utakao wawezesha wajumbe kutoka ngazi ya mkoa kwenda kuingiza mpango katika bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Children in Crossfire, Craig Ferla amesema programu hiyo kwa kiwango kikubwa inabeba dira na mustakabari wa maisha ya watoto ikizingatiwa na robo ya watanzania ni watoto chini ya miaka minane.