Na Saulo Stephen – Singida.
Zaidi ya Maduka 15, ya wafanyabiashara katika soko kuu lililopo Mjini Singida yameteketea kwa moto ambao bado chanzo chake hajifahamik, tukio ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2025 na kusababisha hasara kwa Wafanyabiashara.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Halima Omari Dendego mapema leo asubuhi amefika katika soko hilo la na kujionea hali ilivyo, ambapo amewataka Wafanyabiashara biashara hao kuwa watulivu kwani Serikali iko nao bega kwa bega.

Amesema, tayari Tume imeshaundwa kwa ajili kufanya tathimini pamoja na kushughulikia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika katika soko hilo, ikiwa ni pamoja na kujua nini hasa Chanzo cha moto huo.
Aidha Rc Dendego amesema kuwa tume hiyo amabayo imeundwa itafanya kazi usiku na mchana kwa muda wa siku saba ili kufanya Tathmini ya mali zote zilizoharika kutokana na moto huo.

Jambo Fm imezungumza na baadhi ya Mashuda wa tukio hilo ambao wamesema miundombinu ya soko hilo imbesabisha Zimamoto kushindwa kuzima moto kwa haraka na kuiomba Serikali kuongeza Magari ya Zimamoto ili kuweza kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.
