Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Moto wa soko la K/Koo ni hujuma

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na kamati aliyoiunda kufuatilia tukio la moto Kariakoo lililotokea hivi karibuni, imebaini kwamba haikuwa ajali bali ni hujuma walizofanyiana wafanyabiashara.

Chalamila ameeleza hayo leo Oktoba 20, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha Moto uliotokea Oktoba Mosi, 2023 Kariakoo jijini Dar es Salaam

Chalamila amesema Kamati imebaini Moto huo haukutokana na ajali, bali ni hujuma za Wafanyabiashara wenyewe ambapo Moto ulianzia katika eneo la Mnadani (Kariakoo Auction Mart) na haukusababishwa na Jenereta kama ilivyodaiwa awali

Ameongeza kuwa “Kamera za CCTV zilizokuwa pembeni ya majengo wakati Moto unaanza zimeonesha Jenereta linalodaiwa kuwa chanzo cha Moto ni zima, linafanya kazi na halikuungua”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *