Watu 112 wamepoteza maisha kutokana na moto ulioanzia katika Msitu eneo la Valparaíso ambapo mamlaka zimetangaza Hali ya Hatari huku zoezi la uokoaji likiendelea.
Inaaminika huo ni moto mkubwa kuwahi kurekodiwa Nchini hapo na waathirika wengi walikuwa wakiishi maeneo ya jirani na eneo hilo na wengine walienda kwa ajili ya kutembelea eneo la Pwani kwa ajili ya mapumziko.
Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, Carolina Tohá amesema idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya maeneo kutofikika kirahisi kutokana na moto huo kuendelea