MOI MBIONI KUANZISHA BENKI YA UVUNAJI WA MIFUPA

Na Gideon Gregory – Dodoma. 

Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo na Mishipa (MOI) imesema itaanzisha benki maalumu ya uvunaji wa Mifupa lengo likiwa ni kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto za Mifupa.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisiya katika mkutano na Waandishi wa habari wakai akielezea mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Amesema utaratibu huo utaanza  mara baada ya Sheria ya upandikizaji wa viungo kupitishwa na Bunge huku akidai Kwa sasa utaalamu wa kutengeneza Mifupa katika maabara hawana.

Kuhusu Mifupa wataipataje,Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema “tunavyovuna figo ndivyo tutakavyofanya kwenye Mifupa lazima iwe vizuri hatuendi Kwenye chumba cha maiti na inapatikana kwa utaratibu maalum.

Aidha amesema kuwa ndani ya miaka minne Taasisi ya MOI imetekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la  kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi kupitia huduma za tiba mkoba katika Hospitali mbalimbali ikiwemo Nyangao ya Mkoani Lindi.

Nyingine ni Hospitali ya Kanda ya kusini (Mtwara), Hospitali ya Mtakatifu Benedikt (Ndanda Mtwara), Hospitali ya Rufaa ya Nkinga (Tabora), Hospitali ya Mnazi Mmoja (Zanzibar) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo jumla ya wagonjwa 44,096 Walihudumiwa na wagonjwa 5,382 walifanyiwa upasuaji.

“Pia, Taasisi imesogeza huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi kupitia huduma ya kliniki Jongefu ya MOI (MOI Mobile clinic) ambapo huduma zimetolewa katika maeneo ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Gongo la mboto, Bagamoyo na Morogoro ambapo jumla ya wagonjwa 2,224 wamehudumiwa.

Pia ameelezea mipango ya baadae ya Taasisi hiyo kuwa ni kuendelea kuboresha huduma zao kwa viwango vya kimataifa, Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao (Rehabilitation centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji jijini Dar es salaam.

Kusogeza huduma katika jengo ambalo lilikua linatumika na Hospitali ya Tumaini upanga ili sehemu ya wagonjwa wa  nje waanze kupata huduma katika jengo hilo na kupunguza msongamano MOI,Kuendelea kusogeza huduma zetu karibu na wananchi katika mikoa ambayo hatujaifikia (Tanga, Ruvuma, Kigoma,Geita, Njombe, Manyara, Mara na Kagera)

Pamoja na Kuanzisha huduma mpya za kibingwa na kibobezi ambazo hazipatikani hapa nchini kama vile ‘Bone Bank’ na matibabu ya ‘Parkinson’s disease’ na kutetemeka ndani ya miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *