Uongozi wa Timu ya Taifa ya Misri umethibitisha kuwa Mshambuliaji wao Mohamed Salah amerejea katika klabu yake ya Liverpool kupatiwa matibabu zaidi baada ya kuumia misuli ya paja katika mchezo dhidi ya Ghana kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
Kufuatia hali hiyo Salah ataukosa mchezo wa leo Januari 22, 2024 dhidi ya Cape Verde na kama Misri itafanikiwa kuendelea na michuano kuna uwezekano wa kurejea kuendelea kuitumikia Timu yake katika michuano ambayo itafikia tamati Februari 11, 2024 Nchini Ivory Coast
Naye Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa wamemrejesha klabuni hapo kwa kuwa si kawaida ya Salah kupata majeraha hayo na ndio maana wameongeza umakini katika matibabu yake.