MO AMTEUWA MAGORI KUWA MWENYEKITI WA BODI SIMBA SC

Rais wa Simba SC na Mwenyekiti wa Bodi wa Klabu hiyo, Mohammed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC huku yeye akiendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais.

Kupitia taarifa yake ya hii leo Septemba 4, 2025 Mo ameeleza kuwa maamuzi yake yanatokana na majukumu yake mengine na hasa mara nyingi kuwa mbali na Simba SC inahitaji kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu, mwenye muda wa kutosha na anaweza kushiriki kwa ukaribu.

Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Ibara ya 41, Mo anayo mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi wa Bodi hivyo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi upande wa Mwekezaji:

Barbara Gonzalez – Mjumbe wa Bodi
Hussein Kitta – Mjumbe wa Bodi
Azim Dewji – Mjumbe wa Bodi
Rashid Shangazi – Mjumbe wa Bodi
Swedi Mkwabi – Mjumbe wa Bodi
Zuly Chandoo – Mjumbe wa Bodi
George Ruhango – Mjumbe wa Bodi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *