MNYAMA APOKEA KICHAPO KWA AL MASRY

Klabu ya Doka ya Simba SC, imepoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya AL Masry ya Nchini Misri.

Mabao ya Al Masry yamefungwa na washambuliaji Mualgeria, Abderrahim Deghmoum dakika ya 16 na Mnigeria, John Okoye Ebuka dakika ya 89.

Timu hizo zitarudiana tena Aprili 9, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wa jumla atakutana na kati ya Stellenbosch ya Afrika Kusini au Zamalek ya Misri katika Nusu Fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *