Winga Willy Essomba Onana amecheka na nyavu mara mbili dakika ya 36 na 38 kufanikiwa kuiwezesha Simba kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wydad AC ya Morocco katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam
Ushindi huo wa kwanza kwa Simba katika Kundi B unaifanya kufikisha pointi 5 ikisaliwa na michezo miwili dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast (ugenini, Februari 23, 2024) na dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana (Machi 1, 2024)