Mndeme: Tutafungia mashirika yasiyofuata maadili yetu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Solomon Mndeme amesema Serikali haitosita kuyachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuyafuta Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yatakayobainika kwenda kinyume na mila na desturi za kitanzania wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 5,2023 wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Mashirikia yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa na kueleza kwamba kila mmoja ana wajibu wa kulinda utu, mila na desturi za kitanzania.

Aidha ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi yake mkoani Shinyanga kuepukana utekelezaji wa miradi inayojirudia katika eneo moja na kutoa agizo kwa wataalamu wa halmashauri zote kuimarisha uratibu wa Mashirika hayo ili kuhakikisha kunakuwa na usawa wa mgawanyo wa rasilimali.

Hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2023, Mkoa wa Shinyanga ulikuwa na jumla ya Mashirika 116 yasiyo ya kiserikali yaliyo na makao yake makuu katika mkoa na mashirika ya kitaifa na kimataifa zaidi ya 29 yanayotekeleza afua mbalimbali mkoani Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *