Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Kishapu huku akisikitishwa na kasi ndogo ya mradi wa ujenzi wa ofisi Na nyumba ya mkuu wa wilaya na kutoa muda wa siku 14 mradi Huo uwe umekamilika.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2023/10/dc2ed756-60f9-4ec5-b441-1aac85b5c771-jpeg.webp)
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Kutoka kwa katibu tawala wilaya ya Kishapu Fatma Khaji mkuu wa mkoa amesema haiwezekani mradi huo ukatekelezwa kwa kipindi Cha mwaka mmoja ikiwa vifaa vyote vinavyohusika na ujenzi wa mradi Huo vimenunuliwa.
Aidha Mndeme amesema baada ya ukaguzi katika jengo la ofisi ya mkuu Wa wilaya amebaini kilichosalia ili kukamilika kwa mradi huo ni taa Na vyoo hivyo haoni sababu za msingi za kutokamilika kwa jingo Hilo na amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili Kufikia tarehe 15 November jengo hilo lianze kufanya kazi.
Ukaguzi huo ni mwendelezo wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ambayo anaifanya katika wilaya zote za mkoa huo ili kujionea miradi Ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za serikali ikiwa ni Utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020.