MMOJA ASAKWA KWA MAUAJI KISA USHABIKI WA SIMBA NA YANGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linamsaka Mtu mmoja Emmanuel Daniel Mabura (33),
mkazi wa mtaa wa Mhandu kisiwani, wilaya
Nyamagana, kwa tuhuma za mauaji ya Mussa Juma Said (34), aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na ushabiki wa mpira na tayaru Mwili wamarehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.

“Mnamo tarehe 19.10.2025, majira ya 1.00 jioni huko mtaa wa Mhandu Kisiwani, kata ya Mhandu, wilaya ya Nyamagana, Mussa Juma Said, alifariki dunia baada ya kuchomwa na kipande cha chupa chenye ncha kali na mtuhumiwa Emmanuel Daniel Mabura, baada ya kuibuka mzozo uliotokana na ushabiki wa mpira wa miguu uliyohusisha timu ya Simba na Yanga, ndipo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo baada y kuzidiwa hoja,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kifuqtia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa wito kwa wananchi kushirikiana kwa kutoa taarifa sahihi zitakazo saidia kumkamata mtuhumiwa aliyetekeleza mauaji hayo na kisha kutoroka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *