Mtu Mmoja anayejulikana kwa jina la Nawabu Yakubu Almasi (36), mfanyakazi wa kiwanda cha sukari Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa ameuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wa kiwanda hicho wakati akiamlia ugomvi wa mlinzi huyo na mfanyakazi mwezake.

Tukio hilo limetokea Oktoba 17, 2023 ambapo marehemu alikwenda kuamulia ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya mlinzi huyo ambaye ni Askari wa Kikosi cha Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza (Shima) na moja ya mfanyakazi aliyezuiliwa kuingia kiwandami hapo kwa sababu ya kutokamilisha vigezo vya kuingia ndani ya kiwanda hicho.
Kamati ya usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima wamefika kiwandani hapo ambapo wameeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na tayari mlinzi huyo anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaid ambapo taratibu nyingine za kisheria zitafuata.