Baraka Benedicto ambaye alikuwa Mlinzi wa Kanisa Katoliki la Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi, amepandishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni na kusomewa shtaka moja la kumuingilia Mtoto wa miaka 14 kinyume na maumbile.
Shtaka limesomwa na Wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ikielezwa mtuhumiwa alitenda tukio hilo Februari 3, 2024 ambapo amekana shtaka hilo na amepelekwa rumande Segerea, na Mahakama imepanga kusikiliza tena shauri hilo Namba Machi 18, 2024.