Mlezi wa Kituo cha kulea Watoto yatima cha Mlandizi, Stephano Maswala (35) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, kwa kosa la kubaka Watoto watano waishio kituoni hapo kwa nyakati tofauti kuanzia Oktoba 2024 hadi Januari 2025.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani humo iliyotoleqa hii leo Februari 8, 2025 imeeleza kuwa, mtuhumiwa alikuwa akiwabaka watoto hao akiwadanganya kuwa anawatengeneza kisaikolojia, ili wasisumbuliwe na wanaume mtaani na waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Taratibu za upelelezi dhidi ya mtuhumiwa huyo zinaendelea na anahojwa kwa kina kwa kushirikiana na Idara nyingine za Serikali na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani.
