Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mkuu Wa Wilaya Ya Shinyanga Aridhishwa Na Uhamasihwaji Wa Wananchi Kujiandikisha Katika Daftari La Makazi

Na Eunice Kanumba


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa usimamizi, utekelezaji pamoja na uratibu mzuri wa uandikishaji wa daftari la makazi kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi novemba mwaka huu.


DC Mtatiro ameyasema hayo kwenye kikao kazi cha uhamasishaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa kilichowakutanisha Wakuu wa Taasisi,wakuu wa idara na vitengo,Kamati ya ulinzi na usalama, watendaji wa kata,maafisa elimu kata,wakuu wa shule, maafisa elimu msingi na sekondari pamoja na waganga wafawidhi ndani ya Manispaa ya Shinyanga.


“Tangu zoezi la uandikishaji wapiga kura serikali za mitaa limeanza mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga Mwl. Kagunze amefanya kila kitu, matangazo kila siku yanapita mtaani,redio zinarusha matangazo kila siku,kwa Manispaa ya Shinyanga kama kuna wananchi hawatajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura yatakuwa ni maamuzi yake binafsi “ amesema DC Mtatiro.


Katika hatua nyingine DC mtatiro amewataka wakuu wa vitengo na taasisi katika manispaa hiyo kuhakikisha watumishi wote walio chini yao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi bora kwa ustawi wa taifa.


Zoezi la uandikishaji wa daftari la wakazi (wapiga kura Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024) limeanza Oktoba 11,2024 ambalo litahitimishwa Oktoba 20,2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *