MKUU WA WILAYA MBOZI AFARIKI DUNIA, RAIS SAMIA AMLILIA…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Ester Mahawe kilichotokea leo tarehe 14.01.2025 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC mkoani Kilimanjaro alipokua akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Mhe. Ester Mahawe. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ninatoa pole kwa familia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi na wananchi wote wa wilaya ya mbozi, ndugu, jamaa na mafariki kwa msiba huu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi amesema Mh. Mchengerwa.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya msiba huu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram ameandika ‘Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.

Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali

pema peponi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *