Kufuatia muda unavyoyoma na homa ya uchaguzi wa Papa kupamba moto, Vatican imesema itazima mawasiliano ya simu ndani ya mji huo isipokuwa Uwanja wa Mtakatifu Petro kuanzia Mei 7, 2025.
Hatua hiyo inatokana na uwepo wa mkutano huo wa siri wa kumchagua Papa ambao unasubiriwa kwa hamu ili kujua ni nani Kiongozi mpya anayefuata wa Kanisa Katoliki Duniani.

Papa Francis alifariki Aprili 21, 2025 siku moja baada ya siku kuu ya Pasaka.