Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mkude ahukumiwa jela maisha

Mahakama Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu Mkude Nziku (20) Mkazi wa Kijiji cha Kihanga Wilaya na Mkoa wa Iringa kutumikia kifungo cha Maisha Jela na fidia ya shillingi Milioni Tano baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka Binti wa kaka yake mwenye Umri wa miaka 11.

Kesi hiyo ilisimamiwa na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa Said Mkasiwa ilikuwa na jumla ya mashahidi wanne akiwemo (Binti aliyedaiwa kubakwa, mama Mzazi wa Binti huyo, Daktari pamoja na Polisi aliyechukuwa maelezo ya awali).

Inaelezwa siku ya tukio Mtuhumiwa aliingia chumbani kwa binti huyo kupitia njia ya Dirisha akamchukua mtoto huyo kwa nguvu kutoka kitandani akamuweka chini kisha kumvua nguo zake na kutenda unyama huo.”Alinivua sketi akaivuta nguo yangu ya ndani akaniingiza ‘LIDUDE’ lake sehemu ya kukojolea nilihisi maumivu makali nikapiga kelele mama akaja chumbani kwangu lakini Mkude akakimbia” Alisema Binti huyo

Naye shahidi wa pili ambaye ni mama Mzazi wa mtoto huyo anasema baada ya kusikia kelele za mwanaye alitoka haraka hadi chumbani kwa mwanaye akapishana na mtu sebuleni alianza kumkimbiza punde mtu huyo aliyemtaja kama Mkude akaanguka chini akammulika na taa yake ya Solar na kumtambua, akamuuliza ulikuwa unafanya nini chumbani kwa binti yako (Mtoto wa kaka yake) Mkude akadai kuwa alikosea nyumba kisha akakimbia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *