Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 anayefahamika kwa jina la Hasna Bakari mkazi wa mtaa wa Mazengo kata ya Chang’ombe Jijini Dodoma ametoroka nyumbani kwake baada ya kuzidiwa na mikopo maarufu kama vikoba.
Akizungumza na Jambo Fm nyumbani kwake mume wa mwanamke huyo Nuru Hassan amesema kuwa mama huyo amekuwa akichukua mikopo pale anapotoka kwenda kwenye shughuli zake ili hali mwanamke huyo hana kazi yoyote anayofanya ya kumuingizia kipato.
Aidha ameongeza kuwa hiyo ni mara ya tatu mwanamke huyo anachukua mikopo na akishindwa kulipa anakimbia jambo lililomfanya bw. Hassan kuitafuta Jambo Fm ili aweze kupatikana na kurudisha fedha hizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mazengo Abdallah Ally amethibitisha kupokea taarifa hizo na kuwaomba wanaotoa huduma kuwashirikisha watu wote katika utoaji wao wa huduma kwani wakinamama ndiyo wamekuwa akiathirika pakubwa na suala la mikopo.
Aidha mwenyekiti huyo ametoa ushauri kwa wanaokoposha kuwa wawazi katika kuelezea ukweli juu ya athari zinazoweza kujitokeza na kuweza kuwashirikisha wenza wao.
Naye afisa mtendaji wa mtaa huo Geofrey Nkinda amesema kuwa moja kati ya madhara ya natoweza kujitokeza katokeza kwa wale wanao chukua mikopo kiholela ni pamoja na kupoteza mali zao na kufilisiwa.