MKOPO WA BILIONI 51.42 WATOLEWA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI GEITA.

Na Frank Aman, Geita.

Kiasi cha Sh51.42 Bilioni zimetolewa kama Mikopo kwa Wachimbaji Wadogo wanaofanya shughuli zao za Uchimbaji wa Madini wapatao 226 ndani ya Mkoa wa Geita na maeneo mengine kwa kipindi cha July 2024 Hadi Marchi 2025.

Akizungumza Siku ya Leo katika Hafla ya kufunga Mafunzo ya Kukuza Ujuzi kwa Wafanyakazi ambao ni Wachimbaji Wadogo Manispaa ya Geita, Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Geita, Bw. Titus Kaguo amewataka Wachimbaji hao wajiunge katika Vikundi ili wawezesha kupata Mikopo yenye Riba nafuu katika Sekta hiyo ili kuwawezesha kuwa Nyenzo zitakazo wasaidia katika Shughuli zao za Uchimbaji wa Madini.

Katika Mafunzo hayo yaliyo endeshwa kuanzia June 23 na kumalizika July 5, Mwaka huu katika Mkoa wa Geita, Kaguo amesema kuwa Mafunzo hayo yatawasaidia kuweza kuendesha Shughuli zao za Uchimbaji Madini huku wakitumia Nyenzo za Kisasa kupitia Mitaji inayotolewa na Mfuko wa Hazina.

“Mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa kuzingatia Usalama mahala pa kazi na kuepukana na ajali zinazotokea katika maeneo mengi ya Migodi Nchini,” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Patrobas Katambi ambaye alizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Madini, Steven Kiluswa aliyetegemewa kuwa Mgeni rasmi wa Hafla hiyo amewataka Wachimbaji wajiunge katika Vikundi ili kuwawezesha kupata Mikopo ya kuendeshea Shughuli zao za Uchimbaji Madini ili kuweza kunufaika kwa kiasi kikubwa katika Sekta hiyo.

“Sekta ya Madini inayochangia zaidi ya Shilingi 1.7 Trilioni kwenye Pato la Taifa kwa Mwaka 2023 ambapo katika Kipindi cha Awamu ya Sita kumekuwa na Mageuzi Makubwa na Mafanikio katika Sekta ya Madini ambapo mchango wa Sekta hiyo umeweza kuongezeka kutoka Asilimia 9.1 kwa Mwaka Jana Hadi kufikia Asilimia 10.1 kwa Mwaka huu,” amesema.

Amesema kuwa kiasi cha Sh1.07 Trilioni kimechangiwa katika Sekta ya Madini ambapo kiasi cha Tani6.84 za Dhahabu zenye thamani ya Sh4 Trilioni ziliuzwa na kuifanya Tanzania kuwa Nchi yenye Dhahabu safi iliyosafishwa ambayo imehifadhiwa Bank Kuu ya Tanzania.

Akizungumzia Mafunzo hayo, Katambi amesema kuwa yamelenga kuwapatia Ujuzi Wachimbaji hao hususani Wanawake kuweza kupata Ujuzi wa nadharia ambapo wanufaika wapatao 479 walipatiwa Mafunzo hayo ikiwa na Lengo la kuhakikisha Wachimbaji Wadogo wanakuwa Hadi kuweza kufikia Wachimbaji wa Kati ambapo ameongeza kuwa Shughuli za Wachimbaji Wadogo zitatumiwa na kuchangia Asilimia 40 ya Maduhuli ya Madini Nchini.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Bi. Alana Nchimbi amesema kuwa Sekta hiyo imewezesha kutoa Fursa za ajira zipatazo 8.84 Milioni kupitia Miradi mbali mbali ikiwemo Sekta ya Madini na Miradi mingine ya kimkakati kama Relief ya Mwendokasi (SGR) huku ajira zipatazo 83,000 zimepatikana kupitia Sekta ya Uchimbaji wa Madini ambapo kupitia Programu ya kuwawezesha Wachimbaji Wadogo iliyoanzishwa 2016 kiasi cha Sh11.3 Bilioni zimetolewa katika Programu hiyo ya kuwajengea Ujuzi ikiwa na Lengo la kuimarisha uwezo wa Wachimbaji Wadogo ili kuongeza Ujuzi na Usalama kazini.

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Deusdedith Rutazah ameongeza kuwa wataendekea kuwasilisha Mishahara ya Wafanyakazi wa Taasisi hiyo ambayo ni Asilimia 3.7 ya Makusanyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *