Mkoa wa Geita umetakiwa kuendelea kuhamasisha ushiriki wa uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wadau mbalimbali wa uchaguzi Mkoani Geita kushiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi kujitokeza katika uboreshaji wa taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kujiweka tayari katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jaji Jacob Mwambegele wakati akizungumza na na wadau wa uchaguzi Mkoani Geita katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kupeana taarifa mbalimbali za maandalizi ya kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura hivyo wadau hao wanawajibu mkubwa wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema kupitia zoezi hilo Mkoa wa Geita unatarajia kuandikisha wapiga kura wapya zaidi ya laki mbili na elfu tisini na tisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 24.7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *