Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mke na mume wafarki ajali ya Boda Boda

Watu wawili ambao ni mtu na mke wake wamefariki dunia , baada ya pikipiki waliyopanda kuacha njia na kugonga gema katika Mlima Kinombedo ,uliopo kijiji cha Mkwiti ,wilaya ya Newala, mkoa Mtwara majira ya saa moja asubuhi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo, amesema pikipiki iliyopata ajali ni aina SUN LG yenye namba za usajili MC 828 BUT ,huku chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kumudu pikipiki hiyo.

Kamanda Katembo amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Ismail Hajili Chitapwidi, na mkewe ni Aisha Bakari Chilambo ambapo ametoa rai kwa watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kuwasihi abiria kuvaa kofia ngumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *