Mke amuua mumewe kumnusuru mtoto

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia, Tressfolina Nkolongo (33) mkazi wa mtaa wa Mji Mwema uliopo Halmashauri ya Mji ya Njombe kwa tuhuma za kumuua mume wake Bosco Mhagama (53) kwa kumpiga na nyengo kichwani.

Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo, ambapo Amesema tukio hilo limetokea Oktoba 16, mwaka huu majira ya saa tano usiku.

Amesema chanzo cha mwanamke huyo kumpiga mume wake kwa nyengo kichwani inadaiwa kuwa alikuwa anamzuia marehemu asiendelee kumpiga mtoto wake ambaye alikuwa akimuadhibu.

Amesema jeshi hilo litamfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo wakati wowote baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika ili taratibu za kisheria ziweze kufuatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *